Historia ya AL-HAJI ABOUD JUMBE MWINYI
Historia ya AL-HAJI ABOUD JUMBE MWINYI Mwasisi wa serikali tatu Tanzania Na Yahya Abdullah Khamis (Yahya MAKAMO) Namfananisha Aboud Jumbe Mwinyi na aliyekuwa Rais wa Urusi (1990 – 1991), Mikhail Gorbachev, mwanzilishi wa sera ya ‘Glasnost (sera ya uwazi) na Perestroika—mfumo mpya wa kisiasa na kiuchumi. Gorbachiev alipojaribu kuleta sera hiyo, alipingwa vikali na wahafidhina ambao walizoea kuhodhi madaraka na upangaji wa mambo ya biashara, uchumi na kuikandamiza demokrasia. Pamoja na Jeshi la Urusi kumpindua na kumweka kizuizini, Gorbachev alirejeshwa madarakani kwa nguvu ya wananchi ambao walifanya maandamano ya kumunga mkono. Jumbe aliteuliwa kushika nafasi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, baada ya kuuawa kwa Rais Abeid Amani Karume, mnamo Aprili, 1972. Alianza kuonesha nia ya mabadiliko mara alipoingia madarakani kwa kuachana na siasa na sera za mabavu za mtangulizi wake na kuwafanya wananchi wa Zanzibar waanze kupumua na kujisikia huru z...